Waziri kutoka Kongo avutiwa na utalii Tanzania

0

WAZIRI wa Mazingira wa Jamhuri ya Kongo na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Tabianchi ya Bonde la Kongo (CBCC), Arlette Soudan – Nonault ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jinsi inavyovitunza vivutio vyake vya utalii.

Nonault ambaye pia amewahi kuwa Waziri wa Utalii wa nchi yake aliwasili nchini mapema wiki hii akiambatana na wajumbe nane wa Kamisheni ya Tabianchi ya Bonde la Kongo (CBCC) kwaajili ya kikao na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kitakachoanza kufanyika leo Septemba 11, 2024 jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya ziara yake katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyopo mkoani Manyara, Nonault alisema amevutia na namna Tanznaia inavyoendesha sekta ya utalii nchini kwa kuvitunza vivutio vya utalii na kuvutia watalii kutoka nchi mbalimbali bila kusahau uwekezaji.

“Nimefurahishwa sana kuona Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire ni mwanamke, nimeona uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali lakini pia sekta binafsi, hii ina maana kubwa katika jamii na taifa kwa sababu unachochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii.

“Nimeona wanyama wengi akiwemo Simba, nimeona uwekezaji uliofanywa na Hoteli ya Sofa iliopo ndani ya Hifadhi, hakika uwekezaji wowote wa utalii lazima ufuate sera ya utalii endelevu wa utalii ili kulinda na kuhifadhi mazingira, kwa hili naipongeza sana Serikali ya Tanzania,” alisema.

Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof Dos Santos SIlayo na mratibu wa Mkutano wa Kamisheni ya Tabianchi ya Bonde la Kongo nchini na safari hiyo ya utalii anasema aliamua kumwandalia mgeni huyo safari hiyo ili kumuwezesha mgeni huyo kujionea jinsi Serikali inavyofanya jkkazi kubwa katika kuhifadhi maliasili zake.

“Nimefurahi kuona umevutiwa na hali ya uhifadhi inayoendelea nchini, mafanikio hay ani matokeo ya ongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kasi ya mafanikio ya uhifadhi na sekta ya utalii imeongezeka kutokana na msukumo na hamasa aliyoiweka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuingia uwandani kuvitangaza vivutio tulivyonavyo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania,” alisema.

Akimuaga mgeni huyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi na Mkuu wa hifadhi ya Taifa Tarangire, Beatrice Kessy alimpa zawadi mbalimbali na kumuomba akawe barozi mzuri wa uhifadhi na utaliii huku akimtaka kurejea akiwa na familia yake kutalii zaidi katika hifadhi hio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here