RAIS wa Namibia Hage Geingob amefariki dunia akiwa na miaka 82 kutokana na maradhi ya saratani yaliyokuwa yanamsumbua.
Shirika la Utangazaji la Al-Jazeera imeripotiwa kuwa Hage amefariki dunia leo jumapili katika hospitali ya Lady Pohamba akiwa amezungukwa na mke pamoja na watoto.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Taifa hilo Nangolo Mbumba ametoa taarifa ya kifo hicho kupitia ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa Facebook wa Hage Geingob na kuwataka raia wa nchi hiyo kutulia wakati Serikali ikifanya taratibu za mazishi.