UWT yawapiga ‘Stop’ wasaka Urais Z’bar

0

Na Subira Ally

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewashukuru viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kuthamini kuandaa mkutano uliojumuisha Wanawake kutoka sehemu mbalimbali nchini ikiwemo mikoa yote ya Tanzania bara.

Dkt. Mwinyi amesema hayo katika mkutano wa kumpongeza kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake ulioandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika viwanja vya Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Abdulrahman Kinana ampongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kuimarisha umoja, mshikamano na utulivu wa nchi na kuwaletea maendeleo Wazanzibari.

Alisema, katika miaka miwili iliyobaki utekelezaji wa miradi ya maendeleo utakuwa mkubwa zaidi na Zanzibar baada ya miaka 10 itakuwa ya maendeleo makubwa.

Naye, Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda amesema UWT wameridhika na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 kwa kuvuka malengo ya utekelezaji ndani ya miaka mitatu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa Zanzibar na kuwataka wanaotamani urais kumuachia nafasi Dkt. Mwinyi.

Vilevile, ameeleza kuwa UWT watamchukulia na kumjazia fomu ya kuomba Urais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi pia watafanya hivyohivyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan mwaka 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here