WIZARA ya Mawasilano na Teknolojia ya Habari kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na Tume ya TEHAMA (ICTC), imeendelea na mafunzo ya TEHAMA kwa vitendo kwa wasichana wa shule za Msingi mkoani Morogoro.
Jumla ya wasichana 25 wa shule ya Msingi Saba saba B na Carmel Mkoani Morogoro wanashiriki mafunzo hayo ya siku tano wakifundishwa kwa vitendo kuhusu Akili Unde( AI), teknolojia ya roboti na mtandao wa vitu (Robotics and IoT).
Kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA 2026 ni “Akili Unde kwa Maendeleo: Wasichana Wakibadilisha Mustakabali wa Kidijitali.”