MINARA 749 kati ya 758, sawa na asilimia 98.81, tayari imewashwa na kuanza kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, hatua inayodhihirisha mafanikio makubwa ya Serikali katika kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano hususan vijijini na maeneo yenye changamoto ya mtandao.
Mradi huu unatekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na makampuni ya simu, ukiwa na lengo la kupanua wigo wa mawasiliano, kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, pamoja na kuwawezesha wananchi kunufaika na huduma muhimu kama elimu, afya, biashara na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao.