Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Wakala wa Majengo Zanzibar Mhandisi Mohammed Aboud Mohammed
Na Rahma Khamis, MAELEZO
WANANCHI wametakiwa kufuata taratibu, kanuni na Sheria za ujenzi Ili kuipunguzia gharama Serikali wakati inapotaka kufanya miradi ya Maendeleo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi WAKALA Wa Majengo Zanzibar Mhandisi Mohammed Aboud Mohammed ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kando ya kikao cha Bodi hiyo kilichofanyika Ofisi za ZBA Amani viwanda vidogovidogo.
Amesema, uzoefu unaonesha kuwa watu hujenga bila idhini wala vibali Rasmi vya Serikali Jambo ambalo linaleta athari mbeleni sio tu kuharibu ardhi lakini pia inaigharimu Serikali na kutumia fedha nyingi kulipa fidia Kwa wananchi waliojenga kwenye maeneo yaliopangwa Kwa ajili ya mieadi ya maendeleo.
Aidha amempongeza Dk Mwinyi Kwa Kazi anayoifanya Katika kuleta Maendeleo ya Nchi na Kuleta maisha Bora wazanzibar na watanzania Kwa ujumla.
Ameeleza kuwa Bodi hiyo itaendelea kutoa ushauri kwa Serikali na kusimamia katika kuhakikisha miradi hiyo inafanikishwa Kwa Kiwango chenye ubora katika masuala mbali mbali ya Ujenzi wa miradi ya kimkakati inayoleta mabadiliko ya Kimaendeleo Nchini.
Ameongeza kuwa miradi inayotekelezwa inatoa nafasi kubwa ya ajira na shughuli mbalimbali za maendeleo kutokea na kuwezesha shughuli za uchumi na Kukuza kipato cha mtu kutokana na harakati mbalimbali.
Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa wataendelea kusimamia maeneo yote ya majenzi ya Miradi mbalimbali kuhakikisha
ujenzi unafanyika Kwa utaratibu mzuri na kukuidhi viwango vunavyotakiwa kimataifa na ubora WA Hali ya juuu
Mkurungezi Mtendaji WAKALA WA majengo Zanzibar Mhandisi Kassim Ali Omar aliishauri Serikali kuwafanyia upembuzi yakinifu baadhi ya wakandarasi na washauri elekezi wanaoshindwa kwenda sambamba na Serikali na kupelekea kutofikia malengo yiyokusudiwa kwa wakati sahihil.
“Serikali kuwaangalia vyema wakandarasi na washauri elekezi wenye Tabia za kuharibu miradi ya Serikali kwa Kuchelewesha kukamilisha miradi na kufanya miradi isiyo na viwango.”alisema
Aidha alieleza kuwa Katika miradi wanayoisimamia watahakikisha majengo yote yanakuwa na mazingira rafiki kukuidhi mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum
Bodi ya Wakurugenzi WAKALA WA Majengo Zanzibar imeanzishwa 2017 kwa lengo la kusimamia na kushauri Serikali katika majenzi.