SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeendelea kuonesha ukuaji imara wa kifedha unaoendana na mageuzi makubwa ya sekta ya makazi nchini.
Taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa mtaji wa Shirika umeongezeka hadi kufikia Shilingi Trilioni 6.4, ukilinganisha na Trilioni 5.04 mwaka 2021.
Ukuaji huu ni matokeo ya usimamizi makini, ubunifu wa kifedha na utekelezaji wa miradi mikubwa ya makazi na biashara kote nchini.
Kila jengo jipya linalokamilika limekuwa chanzo cha mapato, ajira na thamani ya kudumu kwa taifa.
Kwa ongezeko hili, NHC inajidhihirisha kama taasisi imara ya kiuchumi — si tu mjenzi wa nyumba, bali mjenzi wa uchumi wa taifa.
“Kila mradi unaotekelezwa ni uwekezaji wa thamani. Kila mafanikio ya kifedha ni ushahidi wa dira sahihi ya maendeleo.”