SMZ yapokea gawio la Bilioni 10 kutoka PBZ

0

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imepokea gawio la Shilingi Bilioni 10,054,000,000 kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa mwaka wa fedha unaoishia Desemba 2024.

Akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa Hisa uliofanyika katika Ofisi za PBZ Mperani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Saada Mkuya Salum, alisema kiasi hicho ni sehemu ya faida iliyopatikana kutokana na operesheni mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.

Ameeleza kuwa PBZ imeendelea kuwa kinara katika ulipaji wa kodi kwa Zanzibar, ambapo kwa mwaka wa fedha 2024 pekee imelipa kodi zaidi ya Shilingi Bilioni 44.3.

Aidha, Waziri Saada alisema gawio la Serikali limeongezeka maradufu kutoka Shilingi Milioni 7 mwaka 2023 hadi kufikia zaidi ya Shilingi Bilioni 10 mwaka 2024, hatua ambayo inadhihirisha uimara wa benki hiyo.

โ€œMatokeo haya ni kielelezo cha utekelezaji wa hatua mbalimbali za kiutendaji, kiuchumi pamoja na maelekezo ya kimkakati yanayotokana na sera ya Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi,โ€ alisema Waziri Saada.

Alisema, PBZ inaendelea kubaki miongoni mwa benki 10 bora nchini Tanzania na imekuwa taasisi ya kuaminika katika ushindani na utoaji wa huduma za kifedha Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Waziri Saada alibainisha kuwa PBZ imepanga kuendeleza upanuzi wake kwa kufungua matawi mapya katika mikoa ya Morogoro, Mwanza, Tanga na Arusha, sambamba na kuboresha huduma zake kwa kuweka mashine mpya za ATM na kufanya matengenezo katika maeneo mbalimbali.

โ€œPBZ imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo na itaendelea kutoa huduma kwa kuzingatia misingi ya kisheria na kuunga mkono juhudi za Serikali zote mbili katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zaidi,โ€ alisisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PBZ, Fahad Hamd Soud, alisema tayari mazungumzo yameanza na Serikali ya Comoro kwa ajili ya uwekezaji, ikiwa ni sehemu ya kuipanua benki hiyo kimataifa.

Aidha, ameeleza kuwa PBZ imeimarisha mifumo yake ya ulinzi na usalama wa fedha za wateja kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha huduma inatolewa kwa usalama na ufanisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here