Wahariri watakiwa kuitumia kwa usahihi Teknolojia ya Akili Unde

0

KATIBU wa Jumuiya ya Viongozi Wanawake duniani (WPL), Neema Lugangira ameshauri wahariri kuhakikisha wanatumia kwa usahihi teknolojia ya Akili Unde (AI) wakati wa Uchaguzi Mkuu kuepusha madhara katika vyombo vya habari.

Akitoa mada ya ‘Uchaguzi Mkuu na Matumizi ya AI’ kwenye mkutano wa kawaida wa TEF, jijini Dar es Salaam Agosti 18, 2025 amesema, katika uchaguzi kuna taatifa nyingi potofu, hivyo AI inaweza kutumika vizuri kuhakiki usahihi wa taarifa.

“Kuna faida nyingi za kutumia AI ikiwemo kusaidia kuhakiki taarifa kwa haraka, kufuatilia kauli za uchochezi hata uchambuzi wa data,” alisema.

Neema alisema, licha ya AI kuwa na matumizi makubwa kwenye dunia ya sasa, pia hutumika kupotosha jamii sambamba na kuharibu heshima ya mtu / mgombea katika jamii.

Amesisitiza kwamba, vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kulinda maadili katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here