UCSAF yaendelea kuwafikia wananchi vijijini

0

MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeendelea na jitihada za kutoa elimu kwa umma katika maeneo ya vijijini, kwa lengo la kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi ya mawasiliano, hususani mradi wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano.

Elimu hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kuelewa thamani ya uwekezaji unaofanywa na Serikali kupitia UCSAF katika kufikisha huduma za mawasiliano kwenye kata 713 zilizopo katika mikoa yote nchini.

Kupitia kampeni hii ya elimu kwa umma, wananchi wanapata nafasi ya kujifunza kuhusu faida za minara hiyo, matumizi salama ya huduma za mawasiliano, pamoja na nafasi walizonazo kushiriki na kufuatilia maendeleo ya miradi katika maeneo yao.

Aidha, elimu hii inasaidia kuongeza ushirikiano kati ya wananchi, Serikali za Mitaa na wadau mbalimbali katika kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi na kuleta tija iliyokusudiwa.

UCSAF inasisitiza kuwa huduma bora za mawasiliano ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, na hivyo itaendelea kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya kunufaika na uboreshaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here