Na Jacquiline Mrisho โ MAELEZO
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba amesema kuwa hesabu za awali za mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2026 zinaonesha kuwa thamani ya Mfuko imefikia zaidi ya Shilingi Trilioni 11.6, thamani ambayo imeendelea kuwa chachu katika uwekezaji wa kimkakati unaolenga kuongeza thamani ya fedha za wanachama.
Mshomba ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habarฤฑ Julai 17, 2026 jijini Dar es Salaam kuhusu msamaha wa tozo kwa waajiri wenye malimbikizo ya michango na tozo itokanayo na ucheleweshaji wa michango.
Ameeleza kuwa ukuaji huo umetokana na ongezeko la michango ya wanachama, uwekezaji wenye tija, maboresho ya mifumo ya utoaji huduma pamoja na matumizi ya teknolojia katika kuongeza ufanisi wa shughuli za Mfuko na kusisitiza kuwa Mfuko huo utaendelea kushirikiana kwa karibu na waajiri, wafanyakazi na wadau wote kuhakikisha mfumo wa hifadhi ya jamii nchini unaendelea kuwa jumuishi, endelevu na wenye kuleta manufaa kwa Watanzania wote.
โKatika kuhakikisha fedha za wanachama zinaendelea kuzaa thamani na kuchangia maendeleo ya Taifa, NSSF imeendelea kutekeleza uwekezaji wa kimkakati unaolenga kuongeza thamani ya fedha za wanachama, kuchochea ukuaji wa uchumi, kuongeza ajira na kuunga mkono maendeleo ya sekta mbalimbali za uzalishaji ambapo uwekezaji wa Mfuko umejikita katika maeneo mbalimbali ikiwemo hati fungani, dhamana za Serikali, hisa, miradi ya kimkakati, milki na amana za benkiโ, amesema Mshomba.
Ameongeza kuwa, mafanikio hayo yanatoa wajibu mkubwa zaidi wa kuendelea kusimamia rasilimali za wanachama kwa uadilifu na kuhakikisha mfumo wa hifadhi ya jamii nchini unaendelea kuwa imara, endelevu na wenye manufaa kwa Watanzania wote.