‘ZNZ itaimarisha ushirikiano wake na CUBA’

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina kila sababu ya Kuimarisha Ushirikiano na Cuba kutokana na mchango unaotolewa na nchi hiyo kwa Maendeleo ya Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipozungumza na Rais wa Baraza la Taifa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Cuba Esteban Lazo Hernandez na Ujumbe wake Waliofika Ikulu Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameishukuru Cuba kwa Misaada inayoendelea kuitoa kwa Zanzibar kwani imekua ikichangia kwa Kiasi kikubwa Maendeleo katika Sekta tofauti Hususan Sekta ya Afya na Kuimarisha Ustawi wa Wananchi wa Zanzibar.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi alisema Ujio wa Ujumbe huo ni fursa Muhimu ya kufungua maeneo Mengine ya Ushirikiano ikiwemo Uchumi wa Buluu, Elimu, Utalii, Teknolojia, Utamaduni, Michezo.

Naye, Rais wa Baraza la Taifa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Cuba Esteban Lazo Hernandez ameihakikishia Zanzibar Kuendelea na Ushirikiano na Kupongeza Mabadiliko Makubwa yaliofikiwa na Zanzibar Katika Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Miundombinu ya Barabara, Hospitali na Vituo vya Afya hapa nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here