Ziara ya Rais Samia nchini Uturuki

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Ziara yake Rasmi katika Ikulu Kulliye Ankara nchini Uturuki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika Ikulu Kulliye Ankara nchini Uturuki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakati wakishuhudia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba na kwa upande wa Uturuki Rais wa Baraza la Elimu Profesa Dkt. Erol Ozvar wakitia saini Makubaliano ya Ushirikiano katika Nyanja ya Elimu ya Juu baina ya Tanzania na Uturuki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakati wakishuhudia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Lela Muhamed Mussa pamoja na Rais wa Baraza la Utalii la Jamhuri ya Uturuki Abdullah Eren wakisaini hati za makubaliano kwa ajili ya kuanzisha ufadhili kwa wanafunzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Uturuki wanaohitimu katika Elimu ya Juu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakati wa utiaji saini Hati za makubaliano kati ya Ofisi ya Rais Uwekezaji ya Jamhuri ya Uturuki iliyowakilishwa na Zeynel Kılınç, Makamu wa Rais wa Ofisi ya Rais Uwekezaji ya Jamhuri ya Uturuki na kwa upande wa Tanzania iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji TIC Gilead Teri.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akiongoza ujumbe wa Nchi yake kwenye mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here