‘ZEZE’ moja ya zana muhimu kwa kabila la wagogo

0

Na Mohamed Kazingumbe

TANZANIA ina makabila zaidi ya 120 na yenye tamaduni tofauti kulingana na makabila hayo. Kabila hili limekuwa na zana nyingi za ala za kipekee za kuutambulisha utamaduni wa kabila hilo. Wagogo ni kabila ambalo linatajwa kuwa ni moja ya makabila yenye watu wengi nchini.

Kutokana na kuwepo kwa zana za kipekee za muziki wa asili kama vile Marimba na Zeze; zana hizi zimekuwa zikiwanufaisha kabila hilo na watanzania kwa jumla.

Kufuatia kukua kwa umaarufu wa kabila hilo unaotokana na kufanya biashara ya zana hizo zinazowaingizia kipato, pia zimekuwa kitambulisho kizuri kwa taifa.

Zana hizo ambazo hutengeneza muziki wa asili mzuri na kutumiwa na wasanii wengi kutoa burudani pia zimekuwa zikitengeneza ajira kwa wanaofahamu kutoa funzo kwa watu wenye kupenda kufahamu namna ya kuzitumia.

Dodoma ni Jiji maarufu lenye sifa kedekede ambazo hapana shaka litazidi kuleta faida kwa watu wengine ikiwa ni pamoja na wageni wapenda kufaida uhondo wa ngoma za jamii hii.

Jamaa hawa wanasambaa katika wilaya za Dodoma yenyewe, Kongwa, Mpwapwa, Chamwino na Kondoa ni miongoni mwa wilaya Kongwe, lakini ni wilaya inayokaliwa na watu wa kabila la warangi, lakini ipo ndani ya Jiji la Dodoma.

Wazee fulani niliowahi kuzungumza nao kutoka Mpwapwa, wanasema mgogo akiwa amebeba zeze lake anaweza kusafiri umbali mrefu huku akivurumisha kifaa hicho bila kuchoka. Wanasema zeze huendana na nyimbo za kikabila zenye maana za faraja na burudani.

Ni kifaa kinachotengenezwa kwa mfano wa mtungi wakinatisha na kibuyu, pia kuna uzi au kamba nyembamba kwa kuleta ngurumo wakati chombo kingine chenye mfano wa upinde kikigusa kamba na kutoa mlio.

Mlio unaotoka kwenye ala hizi mbili, unakuwa kielelezo kamili cha mlio wa zeze. Watumiaji ala hiyo huweza kuleta sauti mchanganyiko zenye kuvutia.

Wagogo ni kabila kubwa lenye wasomi wengi katika historia ya Tanzania, kuna vigogo wa Taifa waliotoka katika kabila hilo tangu uhuru; John Samwel Malecela aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Job Lusinde, yupo pia Job Ndugai, Prof. Palamagamba Kabudi na wengineo wengi. Jambo kubwa zaidi ni jinsi wagogo walivyojizolea umaarufu katika matumizi ya ala ya zeze katika utamaduni wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here