WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia utumishi na Utawala Bora Ridhwani Kikwete jana ameandaa hafla ya kuliombea amani Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wote wanaomsaidia mkuu wa nchi kutekeleza majukumu yao.
Hafla hiyo iliyofanyika jijini Dodoma nyumbani kwa Waziri huyo ilihudhuriwa na mamia ya wananchi wa nafasi mbali mbali wa jiji hilo.
Pamoja na kuliombea Taifa, dua hiyo ilifuatiwa na takrima ya futari kwa waalikwa wote ambao baadhi yao walitoa mwito kwa kila mtu kuimarisha, uzalendo, upendo, uadilifu, mshikamano, kuvumiliana na huruma.