▪️Ni baada ya kuongeza thamani na kufikia Shilingi trilioni 21, Julai 2025
▪️Pamoja na kuongeza ukuaji wa hisa kwa zaidi ya asilimia 246
▪️Asema hatua hiyo ni ishara ya ukuaji imara wa sekta ya mitaji nchini
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amelipongeza Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kuongezeka kwa thamani ya soko hilo na kufikia Shilingi Trilioni 21.0 katika kipindi cha kufikia julai 2025.
Alisema, soko hilo limeongeza ukuaji wa mauzo ya hisa kwa zaidi ya asilimia 246 pamoja na ongezeko la idadi ya wawekezaji hadi zaidi ya akaunti 683,000 ikiwa ni ishara ya ukuaji imara wa sekta ya mitaji nchini
Alieema hayo, Jumanne (Agosti 26, 2025) alipotembelea Ofisi za soko hilo zilizopo Morocco, jijini Dar es Salaam.