Wanafunzi wenye mahitaji maalum wapata viti mwendo Kibaha DC

0

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibaha leo Agosti 7, 2025 imepokea Viti mwendo, vifaa na kufundishia na kujifunzia Kwa watoto wenye uhitaji maalumu.

Vifaa hivyo vimetoka Ofisi ya Rais TAMISEMI vinajumuisha viti mwendo (Wheel Chair) vitano na vifaa vya kujifunzia na kufundishia

Akizungumza wakati wa Halfa ya ugawaji vifaa hivyo kwa walengwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Regina L. Bieda amewataka wazazi Kutunza viti mwendo hivyo ili viwasaidie Walengwa Kwa muda Mrefu.

Bieda amewataka wazazi wenye watoto wenye Changamoto ya ulemavu wasiwafiche ndani badala yake wapelekwe Shule wakapate Elimu kwani ni haki yao ya Msingi.

Kwa upande wake Afisa Elimu Maalumu Msingi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Bi Anna Lulandala amesema viti mwendo na vifaa vingine vitawasaidia katika kuendea kupata Elimu ya Msingi Kwa Wepesi.

Lulandala pia amesema kuna wafunzi 257 wenye Changamoto ya ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ambapo wavulana148 na Wasichana 109.

Naye Afisa Elimu Msingi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Bernadina Kahabuka ameishukuru serikali Kwa msaada huo na kuwataka wazazi kuwapeleka shule Msingi Mlandizi Kwa wenye Ulemavu ili kupata elimu itakayokuja kuwasaidia katika Maisha yao ya baadaye.

Kwa nyakati tofauti Wazazi wenye watoto wenye changamoto ya Ulemavu wameishukuru serikali Kwa kuwakumbuka na kuwathamini watoto wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here