WanaCCM watakiwa kumsemea na kumpigania Rais Samia

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi wanatakiwa kusemewa na kupiganiwa kutokana na mambo makubwa ya maendeleo ambayo wameyafanya hadi hivi sasa.

Akizungumza na wana Jumuiya ya Taasisi ya Mtetezi wa Mama Zanzibar walipomtembelea ofisini kwake jana Aprili 8, mwaka huu, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamisi Mbeto Khamisi alisema wana kila sababu ya kufanya hivyo.

Alisema, Mbeto kuwa mafanikio makubwa yamefikiwa kila sekta na miaka minne ya Dkt. Mwinyi kila mtu shahidi wa maendeleo yaliyofikiwa Zanzibar na miradi ya kimkakati imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 90.

“Wanajitia upofu ambao hawayasemi maendeleo yaliyopatikana,” alisema Mbeto.

Alisema, Mama Samia ametekeleza miradi ya mabilioni ikiwa ni pamoja na Mradi wa Umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ambao aliukuta ukiwa umetekelezwa kwa asilimia 29 na sasa umefikia asilimia 99 na kazi inayofanyika sasa ni kusambaza umeme.

“Tunazalisha umeme wa kutosha ambao tutauza hadi Afrika Kusini” alisema na kuongeza kuwa daraja la Busisi ni mfano mwingine wa kazi kubwa iliyofanywa na Mama Samia na ujenzi wake sasa umefikia asilimia 99.

Alisema, mifano ipo mingi, ununuzi wa ndege 16 ambao unaifanya sasa ATCL kushindana na Ethiopia na Afrika Kusini na haina mshindani Afrika Mashariki.

Alibainisha kuwa, Mama Samia pia ameibeba nchi Kimataifa na mpango wake R nne umeongeza amani na utulivu ambao unazidi kuvutia uwekezaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Msimsemee kwanini? Kuna mtu analalamikia mabango ya Mama Samia, sasa nasema tutayabandika nchi nzima hadi majumbani kwao,” alisema Mbeto.

Mwenezi Mbeto alisema, anawaunga mkono wanajumuia hao ambao Aprili 27 wanaelekea Dodoma na kuwataka watembee vifua mbele kwani kazi za Mama Samia na Rais Dkt. zinaonekana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here