Wadau wa Tasnia ya Habari watakiwa kushikamana

0
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile amesema, licha ya sehemu ya mapendekezo ya wadau kutoingizwa kwenye Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari, bado yaliyomo yanahitajika.
Akizungumza kwenye Kongamano la 12 la Kitaaluma la TEF mjini Morogoro alisema, wadau wa tasnia wanapaswa kuendelea kushikamana na kuepuka mivutano inayoweza kusababisha kutoeleweka.
“Hivi vifungu (katika muswada wa habari) tukisema tuvikatae mpaka pale vyote vitakapopitishwa, tunaweza kuondoka duniani tukiwa hatujavipata,” alisema.
Balile alimweleza Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye alikuwa mgeni rasmi kwamba, asituchoke.
“Tumemwambia Waziri (Nape) hapa Pamoja na kazi aliyoifanya kwenye muswada ule, lakini asituchoke maana tutaendelea kumfuata,” alisema.
Alisema, licha ya Serikali kubadili baadhi ya vifungu, lakini bado kuna vifungu wadau ‘tunapaswa kuendelea kuvidai.’

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here