UCSAF yatoa elimu kwa Machifu wa Mikoa ya Kusini

0

MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umetoa elimu kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa Machifu wa Mikoa ya Kusini na Sekretarieti ya Akida Wabu Development Foundation( AWADEF)

Mafunzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya UCSAF jijini Dodoma, kwa lengo kuwaelimisha viongozi hao wa jadi na wawakilishi wa asasi juu ya majukumu na fursa zinazotolewa na UCSAF katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika maeneo ya pembezoni na yasiyo na mvuto wa kibiashara.

Mafunzo hayo yalilenga pia kuimarisha ushirikiano kati ya UCSAF na wadau wa maendeleo ya jamii ili kuhakikisha jamii mbalimbali nchini, zinapata elimu kuhusu huduma za mawasiliano zinazowezeshwa na Serikali kupitia UCSAF katika maeneo yao.

Akielezea kuhusu mafunzo hayo, Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Kitandu Ugula alisema kuwa, mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za Mfuko katika kujenga uelewa mpana kwa wadau mbalimbali kuhusu vipaumbele vyake, hususan katika kufikisha huduma za mawasiliano maeneo ya vijijini.

Machifu na wawakilishi wa AWADEF, walitoa pongezi kwa UCSAF na kuahidi kushirikiana kwa karibu katika kuhamasisha ulinzi wa miundombinu ya mawasiliano katika maeneo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here