UCSAF wapongezwa kwa kufikisha Mawasiliano Vijijini

0

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Shaban Millao, ametembelea banda la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika Maonesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.

Millao amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali kupitia UCSAF katika kuhakikisha kuwa huduma bora za mawasiliano zinafika maeneo ya vijijini.

Ameeleza kuwa juhudi hizo zina mchango mkubwa katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara.

Aidha, alielezwa kuhusu miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na UCSAF ikiwemo maendeleo ya ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here