UCSAF kujenga minara 280 kufikisha mawasiliano zaidi nchini

0

MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umetangaza kuanza ujenzi wa minara 280 katika awamu ya 10, lengo likiwa ni kuongeza upatikanaji wa huduma za mawasiliano, hasa katika maeneo yaliyokosa huduma hiyo.

Hadi sasa, UCSAF inaendelea na ujenzi wa minara 758 ambao umefikia asilimia 97.36 ya utekelezaji, ambapo ujenzi wa minara mpya utaongeza wigo wa huduma za mawasiliano nchini.

Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Mwasalyanda, amesema kuwa baada ya kukamilika kwa minara 758, ujenzi wa minara 280 utaanza huku akieleza kuwa hatua zote za maandalizi tayari zimekamilika.

Aidha, ameongeza kuwa awamu ya 11 itafuata mara baada ya kumalizika kwa awamu 10 ambayo pia itajumuisha ujenzi wa minara 280.

Miradi yote hii ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za mawasiliano.

UCSAF imeongeza kuwa itaendelea kushirikiana na watoa huduma za mawasiliano, wananchi na wadau mbalimbali ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi wenye tija na endelevu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here