‘Tumieni umeme wa REA kujikomboa kiuchumi’

0
MBUNGE wa jimbo la Ushetu, Emannuel Cherehani

Na Mathias Canal

MBUNGE wa jimbo la Ushetu, Emannuel Cherehani amewataka wananchi kutumia uwepo wa umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kujiletea maendeleo ya kiuchumi.

Mbunge Cherehani ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha SabaSabini, Kata ya SabaSabini Halmashauri ya Ushetu, mkoani Shinyanga.

Alisema, mpaka wakati anaingia kwenye nafasi ya Ubunge Novemba 2021 Vijiji 21 pekee ndio vilivyokuwa na umeme na mpaka Januari 2024 Vijiji 78 kati ya Vijiji 112 tayari vina umeme.

“Tunamshukuru Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan maana anahangaika usiku na mchana kuhakikisha tunapata fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo huu mradi wa kusambaza umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)”

“Njia pekee itakayompa faraja Mhe. Rais ni kuona wananchi wake mnajikomboa kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kupitia umeme huu. Tusitumie umeme huu kuwasha taa pekee, bali tubuni na kufanya miradi ya biashara itakayoinua hali ya vijiji vyetu pamoja na uchumi wetu kama kufungua saluni pamoja na miradi mingine.” alisema Cherehani.

Mbunge Cherehani alisema, Vijiji ambavyo umeme haujafika atahakikisha mpaka Machi mwaka huu miundombinu itakuwa ishafika kwa ajili ya kuanza kunufuaika na umeme wa REA kama vilivyo vijiji vingine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here