Trilioni 3.5 zatumika kuwawezesha vijana kiuchumi

0

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imefanikiwa kutoa kiasi cha Shilingi Trilioni 3.5 kufikia mwaka 2024 kwa ajili ya uwezeshaji wa vijana kiuchumi kutoka Shilingi Bilioni 904 mwaka 2021.

Amesema kuwa fedha hizo zimewasaidia vijana kupata mitaji ambayo imewawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na hatimaye kuinua vipato vyao pamoja na uchumi wa Taifa.

Amesema hayo Oktoba 10, 2025 wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa iliyofanyika mkoani Mbeya. Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.”

Majaliwa amesema Serikali imefanya hivyo kwa kutambua kuwa Vijana ni nguvu kazi na ndiyo msingi wa safari ya maendeleo ya Taifa letu.

“Vijana wakipewa nafasi na kuandaliwa ipasavyo, wanaweza kuwa nguzo kuu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, na kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs)”.

Mheshimiwa Majaliwa ameongeza kuwa vijana wamekuwa nguzo muhimu ya maendeleo katika sekta mbalimbali nchini na wamechangia kwa kiwango kikubwa katika kilimo, biashara, teknolojia, michezo na sanaa.

“Katika nyanja za ubunifu na teknolojia, vijana ndiyo vinara wa matumizi ya teknolojia mpya na majukwaa ya kidijitali, ikiwemo akili mnemba (artificial intelligence) na mifumo ya mawasiliano ya kisasa, Michango yao imekuwa kichocheo cha mabadiliko chanya katika jamii na uchumi wa Taifa.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here