TRA yakusanya Shilingi Trilioni 7.79

0
Kamishna Mkuu TRA Yusuph Mwenda.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 7.79 ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 105 ya lengo iliyokuwa imejiwekea ya kukusanya Shilingi Trilioni 7.42 katika kipindi cha miezi mitatu (Julai – Septemba) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu TRA Yusuph Mwenda alisema, ufanisi huo umefanya kuvuka lengo la kila mwezi kwa miezi yote mitatu.

Alisema, katika kipindi cha mwezi Septemba mwaka wa fedha 2024/25, TRA ilifanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 3.02, sawa na ufanisi wa asilimia 105 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 2.88.

“Makusanyo haya ni ya kiwango cha juu kabisa cha ukuaji wa asilimia 77.6 kuweza kukusanywa na TRA katika mwezi Septemba, ndani ya kipindi cha miaka mitano tangu mwaka 2020/21,” alisema Mwenda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here