Thamani ya Taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina yaongezeka

0
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema thamani ya uwekezaji katika Taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina imeongezeka kutoka Shilingi Trilioni 70 mwaka 2021 hadi kufikia Shilingi Trilioni 76 mwaka 2023 ambayo ni sawa na ongezeko la 8.6%.

Matinyi alisema hayo wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani.

“Sababu ya ongezeko hili ni Serikali ya Awamu ya Sita kuongeza mitaji kwa kiasi cha Shilingi Trilioni 5.5 katika mashirika ya kimkakati kwa maslahi ya taifa,” alisema Matinyi.

Aidha, Matinyi alisema Ofisi pia imeongeza makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi kutoka Shilingi Bilioni 637.66 hadi Trilioni 1.008 kwa mwaka 2023, sawa na ongezeko la 58%.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here