TARURA yaanza utekelezaji mradi wa DMDP-II jijini Dar es Salaam

0

WAKALA ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam imekwishaanza kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara za DMDP Awamu ya Pili katika Wilaya zote za Ubungo ,Ilala, Kinondoni, Temeke na Kigamboni.

Meneja TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga alisema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri wa barabara cha mkoa.

Mkinga alisema, utekelezaji wa miradi ya DMDP umekwishaanza na baadhi ya wakandarasi wapo saiti.

“Miradi ya DMDP iliyosainiwa imekwishaanza toka tarehe 15 mwezi Januari mwaka huu na sasa hivi wakandarasi wote wako ‘site’ wanafanya kazi za awali za uondoaji miuondombinu ya Tanesco na Dawasa ili mradi ukianza kusiwe na usumbufu” alisema Mhandisi Mkinga.

“Hatua nyingi za awali za kimikataba zimefika mwisho sasa tumeingia katika utekelezaji hivyo ni jambo la lazima kuondoa miundombinu mingine ili tuweze kuweka mitambo barabarani,” aliongeza

Hata hivyo, ametaja kuanza kwa ukarabati wa maeneo ambayo yaliathiriwa na mvua za El Nino pamoja na utekelezaji wa miradi midogo midogo katika mkoa huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here