WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita amewataka Wanamitindo kuiwakilisha vyema nchi kwa kutangaza Utamaduni wa Tanzania na lugha ya Kiswahili kwa Ujumla.
Ameyasema hayo, alipopokea akizungumza na Wanamitindo saba (7) kutoka Taasisi ya Miss Grand Tanzania Organization wakati walipofika Ofisini kwake Migombani kwa ajili ya kujitambulisha.
Alisema, Ugeni huo, uliowasili Zanzibar, unaiwakilisha Nchi kwenye mashindano makubwa ya Urembo Duniani hivyo amewataka kutosahau kuitangaza Nchi yao kiutamaduni na kiutalii ikiwemo mavazi ya kanga na Chakula cha asili.
Amewataka Wanamitindo hao, kuitumia fursa hiyo kwa kukuza mahusiano mazuri na mataifa mengine ili kuitangaza Nchi ya Tanzania kiutalii na kiutamaduni.
Hata hivyo, Waziri Tabia aliwataka Warembo hao, kuwaunga mkono Vijana wa Zanzibari ambao wanajishighulisha na Masuala ya faction design ili wapate muamko katika kufuatilia fursa ya kuingia katika mashindano hayo.
Sambamba na hayo alisema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi wamekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono wabunifu mbalimbali ikiwemo wanamitindo ili kuutangaza Utamaduni wa Tanzania kiutalii.
Nae Katibu wa Miss Grand Organization Tumaini Henry, lengo la ziara hiyo ni kuunga mkono maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kudumisha Urithi wa Utamaduni wa Taifa pamoja na kutengeneza Filamu ya makala (documentary), itakayoonesha urithi wa Zanzibar kupitia Sanaa, Michezo na Uamaduni kwa ajili ya matumizi ya kimataifa.
Alisema, Jumla ya Warembo saba, wameibuka ushindi kati ya warembo 24 ambao wamepata fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano makubwa ya Urembo wa Dunia.
Miss Grand Tanzania ni Organization isiyokua ya kiserikali yenye lengo la kuwezesha warembo Wenye ndoto za kushiriki mashindano ya Urembo kimataifa na kuiwakilisha nchi kwa kupitia platform hii wanapata fursa Mbali mbali za kiuchumi pamoja na kuonesha vipawa vyao.