Stars yawapa furaha Watanzania

0

KATIKA mchezo wa kusisimua uliopigwa usiku huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ilikabiliana vikali na timu ya Burkina Faso, imeibuka na ushindi wa 2-0.

Magoli hayo yanakuwa ya kwanza kwenye mechi ya ya ufunguzi wa mashindano ya CHAN 2024.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ndiye mgeni wa heshima katika ufunguzi huu ambao pia umehudhuriwa na Rais wa CAF, Patrice Motsepe, akishuhudia timu hizo zikimenyana katika uwanja huo.

Mashabiki wameujaza uwanja mapema kwa hamasa kubwa, wakipeperusha bendera za Taifa huku wakionyesha imani kubwa kwa kikosi cha kocha Hemed Suleiman (Morocco), kilichokuwa na dhamira ya kupata matokeo mazuri nyumbani.

Magoli hayo mawili yamefungwa na Abdul Suleimani (Sopu) baada ya Taifa Stars kupata mkwaju wa penati kutokana na madhila waliyoyafanya wapinzani wao Burkina Faso, huku goli la pili likifungwa na Mohamed Hussein, dakika ya 74.

Hata hivyo, kukamilika kwa mechi kati ya Tanzania na Burkina Faso sio mwisho wa burudani kwa usiku huu, bali burudani hizo zinaendelea kwenye Tamasha la CHAN SINGELI katika uwanja huo ambapo halitakuwa na kiingilio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here