KIKOSI cha timu ya mpira wa miguu Taifa Stars kimeweka kambi mkoani Dar es Salaam wakijiandaa na ufunguzi wa michuano ya CHAN 2024 itakayozinduliwa Agosti 02, 2025, na mechi dhidi ya Burkina Faso, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo iliyotokea mkoani Karatu imefika katika Uwanja wa Gymkhana usiku huu, Julai 29, 2025, ikiongozwa na mwalimu wao, Kocha Hemed Suleiman.