SMZ kujenga shule 23 za kisasa

0

SHULE 23 zaidi za kisasa za ghorofa zenye vifaa vyote vya vinavyohitajika kwa ajili ya kufundishia, zitaanza kujengwa hivi karibuni Zanzibar.

Shule hizo ni tofauti na zingine 35 za ghorofa ambazo zimejengwa Zanzibar zikiwa na vifaa na maabara za kisasa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya mkopo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 240 na Benki ya CRDB, mjini Zanzibar leo Mei 21, 2025.

Rais Dkt. Mwinyi alisema, shule hizo zitajengwa kule ambako hawana shule za ghorofa kulingana na mahitaji. “hadi Tumbatu wanaenda kupata shule za ghorofa.”

Alibainisha kuwa, mkopo huo ambao ni wa kwanza kwa Zanzibar toka nje ya nchi kupitia benki za ndani, unafungua mapinduzi mapya ya kiuchumi na anawasuta wanaodai kuwa nchi inakopa sana.

Alisema, nchi ina mfuko wa madeni ambao kila mwezi Serikali inaingiza Shilingi Milioni 10 na kiwango cha ukopaji kulingana na pato la Taifa nchi ipo katika asilimia 17 wakati kikomo ni asilimia 50 hadi 53.

“Bado tupo vizuri na hata mkopo huu ambao tumepewa tuulipe baada ya miaka mitano tunaweza kuulipa ndani ya muda mfupi zaidi kama tukiamua kutoa pesa kwenye mfuko wetu wa madeni,” alisema Dkt. Mwinyi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here