SMZ kuendelea kuimarisha miundombinu ya uchumi wa Buluu

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya sekta ya Uchumi wa Buluu ili kuhakikisha wananchi wananufaika zaidi na kukuza kipato chao.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wavuvi, wakulima wa mwani na wananchi katika Bandari ya Mkoani, wakati alipotembelea soko jipya la Mkoani linaloendelea kujengwa, diko, na kukabidhi vifaa kwa wakulima wa mwani pamoja na boti kwa wananchi wa Kisiwa cha Makoongwe, katika hafla iliyofanyika mkoani humo.

Amesema kuwa sekta ya uvuvi na kilimo cha mwani ni miongoni mwa nguzo muhimu katika utekelezaji wa sera ya Uchumi wa Buluu, hivyo Serikali ya Awamu ya Nane inaendelea kuwajengea uwezo wakulima na wavuvi kupitia utoaji wa vifaa vya kisasa, ujenzi wa masoko na madiko, pamoja na mafunzo ya kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao yao.

Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda, ikiwemo kuongezeka kwa mavuno ya mwani na kiwango cha samaki wanaovuliwa kwa sasa.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu ili kuimarisha sekta hizo, ikiwemo diko na soko la Mkoani pamoja na kiwanda cha mwani cha Chamanangwe, kwa lengo la kuwaandalia wakulima mazingira bora ya uzalishaji.

Vilevile, amesema Serikali itaendeleza ujenzi wa miundombinu ya Uchumi wa Buluu katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba, ikiwemo Bandari ya Shumba, soko la Kiwani, na kiwanda cha kusarifu mwani cha Chokocho.

Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa hatua ya makabidhiano ya boti kwa Kisiwa cha Makoongwe itapunguza changamoto za usafiri kwa wananchi, na kwamba kina mama wa Mkia wa Ng’ombe watapatiwa boti ili kuimarisha uzalishaji wa zao la mwani.

Amesisitiza kuwa hatua hizo zote zinalenga kuwawezesha wanawake na vijana kuongeza kipato chao na kunufaika na sekta ya Uchumi wa Buluu, ambayo kwa sasa inawawezesha zaidi ya wananchi 100,000 kujipatia kipato.

Rais Dkt. Mwinyi amewapongeza watendaji wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi kwa kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa dham

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here