Na Mwandishi Wetu
BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetoa rasmi ratiba mpya ya Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2026/2027.
Katika ratiba hiyo, mchezo wa kwanza wa Watani wa Jadi, Simba SC na Yanga SC, unatarajiwa kupigwa Oktoba 10, 2026.
Mchezo huo wa mzunguko wa kwanza utashuhudia Simba wakiwa wenyeji katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ukianza majira ya saa 1:00 usiku.
Hatua hii inafanya timu hizi kongwe nchini kukutana mara sita (6) ndani ya mwaka huu wa 2026 tu.