Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Chukwani, Unguja, Zanzibar kuelekea shamrashara za miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, Januari 5, 2026.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Ofisi ya Makamu wa Rais imeweka mikakati Madhubuti ya kuhakikisha elimu ya Muungano inatolewa zaidi.
Amezungumza hayo Januari 5, 2026 wakati wa Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Chukwani, Unguja, Zanzibar kuelekea shamrashara za miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba.
Masauni amempongeza Waziri Mkuu Dkt. Nchemba pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuisaidia Ofisi ya Makamu wa Rais kutekeleza moja ya mikakati yake ya uenezaji wa elimu ya Muungano kwa wananchi.
“Leo hii tumekuja hapa na tumejifunza kitu na sasa tunakwenda kuboresha mpango wetu wa utoaji elimu na kuwa wa vitendo kwa kuwa leo mmetupa elimu hiyo kwa vitendo,” amesema Masauni.