‘Serikali itaendelea kujenga nyumba za kisasa kwa wananchi’

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewathibitishia Wananchi kuwa Serikali itaendelea Kujenga Nyumba za Kisasa Maeneo yote ambayo yana Nyumba zilizo Chakavu kwa lengo la kuwapatia Wananchi Makaazi bora.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo katika Ufunguzi wa Nyumba 72 za Makaazi na Biashara Mombasa kwa Mchina Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Zanzibar.

Rais Dkt.Mwinyi ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi kuandaa Mpango Maalum wa Kisheria wa Matunzo ya Nyumba inazozijenga ili Suala la Matunzo kuwa la Lazima na Sio hiyari.

Rais Dkt. Mwinyi amefahamisha kuwa Mpango huo ni lazima Uzingatie Mifumo ya Maji, Masuala ya Usafi na Uangalizi wa Nyumba zenyewe Ili ziendelee kuwa na Haiba nzuri ilizonazo hivi sasa.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewashauri Wamiliki wa Nyumba hizo kuanzisha Kamati Maalum za Matunzo ya Nyumba hizo kwa kila Mmiliki kuwajibika na Usafi na Matunzo ya Nyumba anayomiliki.

Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa Wananchi ni lazima Wakubali kupisha Miradi ya Ujenzi wa Nyumba na kwamba Serikali itawafidia Nyumba Bora za Makaazi badala ya Fedha.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Wananchi Kukaa katika Makaazi mazuri ndio dhamira ya Serikali na kuwa Mpango wa Ujenzi wa Nyumba 3000 eneo la Chumbuni utaendelea katika maeneo mengine na kuwaambia Wakaazi wa Kikwajuni kukaa tayari kwani nyumba mia tano zitajengwa katika eneo hilo na Serikali ipo tayari kwa Mradi huo.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuridhika na Utendaji wa Wizara hiyo kwa Mafanikio Makubwa ya Miradi ya Ujenzi wa Nyumba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here