Rais Samia azindua Barabara ya Babati Mjini

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Tamisemi Anjellah Kairuki, pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa barabara za lami za Babati mjini km 8.1 kwenye hafla iliyofanyika Babati Mkoani Manyara tarehe 22 Novemba, 2022.

Na Jumbe Abdallah

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua barabara ya Babati mjini yenye urefu wa Kilomita 8.1 iliyojengwa chini ya Mradi wa Kuzijengea Uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Rais Samia amefanya uzinduzi huo ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya siku mbili Mkoani Manyara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Tamisemi Anjellah Kairuki kuashiria uzinduzi wa barabara za lami za Babati Mjini KM 8.1 kwenye hafla iliyofanyika Babati Mkoani Manyara.

Aidha, mradi wa ujenzi wa barabara hiyo umegharimu Shilingi Bilioni 12.1 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua na taa za barabarani.

Mradi huu wa barabara umejengwa kwa fedha za Mkopo kutoka Benki ya Dunia chini ya Usimamizi wa Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Kwa upande mwingine, Rais Samia pia alizindua Mradi wa vihenge na maghala ya kisasa ya kuhifadhia chakula ya Wakala wa Taifa wa Mradi wa Chakula (NFRA) wilayani Babati mkoani Manyara wenye thamani ya Shilingi Bilioni 19.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuashiria uzinduzi wa Vihenge na Maghala ya Kisasa ya kuhifadhia Chakula katika hafla iliyofanyika Babati mkoani Manyara.

Awali, akiwa njiani kuelekea mkoani Manyara, Rais Samia alisimama na kuzungumza na wananchi wa wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma na baadae kuzungumza na wananchi wa Kata ya Bonga wilayani Babati.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wananchi wa Wilaya ya Kondoa alipokuwa njiani akielekea Wilaya ya Babati Mkoani Manyara kwa ajili ya kuanza ziara ya kutembelea na kukaguwa miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here