Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya utenguzi wa nafasi za Viongozi wafuatao:-
- Bw. Reuben Ndiza Mfune, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali;
- Bw. Msongela Nitu Palela, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Mara;
- Bw. Michael Augustino Matomora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Singida;
- Bw. Linno Pius Mwageni, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Shinyanga; na
- Bw. Sunday Deogratius Ndori, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Njombe.
Utenguzi huu ulianza tarehe 22 Januari, 2023.