Rais Mwinyi: Ziara ya Uingereza imekuwa na manufaa makubwa kwa Z’bar

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa ziara yake Uingereza imekuwa na Manufaa Makubwa kwa Zanzibar kwani Wawekezaji wengi wameonesha dhamira ya kuwekeza Nchin

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipozungumza na Waandishi wa Habari Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Baada ya Kuwasili Nchini akitokea Uingereza alikohudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Madola wa Masuala ya Biashara na Uwekezaji uliojikita katika Agenda ya Uchumi wa Buluu.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi alisema Uchumi wa Zanzibar Umeendelea kukua kila Mwaka ambapo sasa Umefikia zaidi Asilimia 7.

Vilevile, Rais Dkt Mwinyi amefahamisha kuwa Ukuaji huo wa Uchumi utaendelea kukua zaidi kutokana na Juhudi zinazochukuliwa na Serikali za kuwa na Sera Bora na Kuzitangaza fursa pamoja na kuwakaribisha Wawekezaji Zaidi wa Mataifa mbalimbali kuwekeza Nchini.

Halikadhalika Rais Dkt, Mwinyi amezitaja Sekta Tatu kuu za Uchumi ikiwemo Utalii,Uchumi wa Buluu na Utafutaji wa Mafuta na Gesi ndio Sekta za Kipaumbele kwa Serikali ambazo Wawekezaji wengi wamedhamiria kuwekeza na Serikali imewahakikishia Ushirikiano kufanikisha Azma zao.

Amebainisha kuwa Wawekezaji wengi wa Uingereza wameonesha Nia ya kuwekeza katika Kuliongezea thamani zao la Mwani kwa kuongeza Mnyororo wa Thamani pamoja na Uzalishaji wa Mbegu Bora, Utafiti na Kuwajengea Uwezo Wakulima wa Mwani.

Akizungumzia Sekta ya Mafuta na Gesi alisema Kampuni nyingi zimejitokeza ambazo zimeingia Mkataba na Serikali Juu ya Utafutaji wa Data za Mafuta na Gesi na Kuzitangaza Duniani kwa ajili ya Kupata Wawekezaji Zaidi.

Rais Dkt. Mwinyi amewahakikishia Wawekezaji kuwa Zanzibar bado Ina fursa nyingi za Uwekezaji na kukuza Uchumi na Serikali inazitangaza kwa Kiwango kikubwa.

Kuhusiana na Nishati ya Umeme Rais Dkt,Mwinyi amewakaribisha Wawekezaji wa Uingereza kuwekeza Nchini katika Umeme wa Upepo, Takataka na Jua Ili kuiwezesha Zanzibar kujitegemea kwa Nishati Hiyo Muhimu.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Nchi imeanza kuzidiwa na Matumizi Makubwa ya Umeme hivi sasa hivyo Uwekezaji katika Eneo Hilo Lina Umuhimu Mkubwa

Kwa Upande wa Utalii alisema Zanzibar inasisitiza Sera ya Utalii Endelevu na tayari imewaelimisha Wawekezaji kuzingatia Sera Hiyo Hususani Uhifadhi wa Mazingira na kwamba Zanzibar inahitaji Watalii wenye Uwezo watakaoifanya Nchi Kupata Fedha nyingi na sio idadi kubwa ya Watalii .

Akizungumzia Suala la Wazanzibar Wanaoishi nje ya Nchi (Diaspora) Amesema Mchakato wa kuwapatia hadhi Maalum Umefikia pazuri kwani Tayari Umewasilishwa Bungeni Ili Kupata ridhaa ya Bunge Hilo ili nao Wapate fursa za Msingi ikiwemo Ununuzi wa Ardhi, Bima ya Usafiri na kutambulika kwa familia zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here