Rais Mwinyi: Zanzibar ina sera bora kwa uwekezaji

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa ya maendeleo kipindi cha miaka 4 kwa mageuzi katika sekta mbalimbali na kuimarika kwa mifumo pamoja na kuanzisha sera bora kwa uwekezaji zinazolenga kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na Kimataifa.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo katika Jukwaa la Uwekezaji katika Uchumi wa Buluu lililofanyika, Makao Makuu ya Ofisi za Citibank, London Aprili 8, 2025 na kuhudhuriwa na Kampuni mbalimbali za uwekezaji za Uingereza zenye nia ya kuchangamkia fursa za uwekezaji Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi amefahamisha kuwepo kwa Citibank kuwa mshirika mkuu wa maendeleo Zanzibar kutachochea zaidi uwekezaji katika sekta za uchumi wa buluu, nishati pamoja na nyumba na makaazi.

Rais Dkt.Mwinyi amebainisha kuwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma unalenga kuzifanya bandari kuwa za kisasa, uanzishwaji wa viwanda vya usindikaji wa mazao ya baharini.

Vilevile, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa upatikanaji wa fedha utaisaidia Serikali kuendelea kuwawezesha Wanawake wakulima wa Mwani, wavuvi na vijana katika mafunzo ya ujuzi mbalimbali.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito katika jukwaa hilo kuwekeza katika sekta ya uvuvi na ufugaji wa samaki, utalii wa mazingira, na uhifadhi wa baharini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here