RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuwa tayari kuwasaidia Maimamu na Walimu wa Madrasa kwa hali na Mali ili wawe na hali Bora za kimaisha na kuendelea kufundisha Elimu ya Dini kwa Ufanisi.
Rais Dkt.Mwinyi alisema hayo alipoufungua Msikiti wa Almaghafira uliopo Nungwi Kidimni, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu amewahimiza Kuutumia Msikiti huo kwa Kusali kwa Bidii pamoja na kuandaa Utaratibu Mzuri wa Kuutunza ili ubaki kuwa na Mazingira mazuri wakati wote.
Msikiti wa Almaghafira uliojengwa kwa Nguvu za Waumini na Wahisani mbali mbali.