Rais Mwinyi: Tuongeze fursa za uwekezaji katika mafuta na gesi

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kuongeza fursa za uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi ikiwemo uanzishwaji wa mfuko wa mafuta, utekelezaji wa miradi ya mipakani pamoja na kuongeza ubunifu wa kiteknolojia katika sekta hiyo.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipofunga Kongamano la 11 na Maonesho ya Petroli Afrika Mashariki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere ( JNICC), Dar es Salaam Machi 7, 2025.

Aidh, Rais Dkt.Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake thabiti ya kuendeleza sekta zote za uchumi.

Alieleza kuwa, chini ya uongozi wake maendeleo makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa miradi ya kitaifa na kimkakati ikiwemo sekta ya mafuta na gesi.

Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi alisema maendeleo ya kiteknolojia ni muhimu kwa sekta ya mafuta na gesi kwa kutambua kwamba dunia inakwenda kwa kasi katika masuala ya uvumbuzi ili kuoanisha na sekta hiyo.

Vilevile, Rais Dkt.Mwinyi amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Nchi washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kukuza fursa za uwekezaji katika sekta ya petroli kwa ajili ya utafutaji ikiwemo uchunguzi na ugunduzi zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here