RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itahakikisha kuwepo kwa utii wa Viongozi katika utendaji wa Taasisi za Umma ili kuepusha mifarakano baina ya Watendaji
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipozungumza katika Kongamano la Pili la Kiimani kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika Ukumbi wa Idrissa Abdulwakil Kikwajuni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 23 Machi 2025.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa amekuwa akipokea Taarifa nyingi za kuwepo kwa ugomvi katika Taasisi za Umma baina ya Watendaji wenye dhamana jambo ambalo Serikali inadhamiria kuliondosha.
Akizungumzia Kuhusu Amani Rais Dkt.Mwinyi amesema ndio suala muhimu zaidi katika Nchi na kila Mmoja kwa nafasi aliyonayo anapaswa kuhubiri Amani.
Halikadhalika , Rais Dkt.Mwinyi alisema kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa hapa Zanzibar kunalenga kudumishwa kwa Amani na kuwanasihi Wanasiasa kushirikiana na Serikali kufanikisha Azma hiyo kwa manufaa ya Nchi.
Kwa upande mwingine, Rais Dkt.Mwinyi ameishukuru Afisi ya Mufti Mkuu kwa kusimamia Vizuri na Kuendeleza Mambo yote ya Dini ya Kiislamu ikiwemo Kongamano Hilo la Kiimani kwa Viongozi wa Serikali.