Rais Mwinyi: Miaka 61 ya Muungano, Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania imepiga hatua kubwa za Maendeleo ndani ya Miaka 61 ya Muungano Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii na kuwa kielelezo cha Mafanikio ya Muungano Barani Afrika.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipoweka jiwe la Msingi la Ujenzi Wa Barabara ya Kibada-Mwasonga Wilaya ya Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Rais Dkt Mwinyi alisema Wananchi wa pande zote mbili wanaendelea kunufaika na matunda ya Muungano tangu Kuasisiwa kwake na kufanikisha dhamira ya Waasisi wake
Ya Kuleta Uhuru, Umoja na Maendeleo ya Watanzania.

Rais Dkt. Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea Kuimarisha Muungano kwa kuzipatia Ufumbuzi Changamoto za Muungano kwa kupitia vikao vya Pamoja vya Majadiliano kama ilivyofanywa na Viongozi waliopita.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amefafanua kuwa Amani ya kudumu na Umoja wa Watanzania ni Tunu Muhimu zinazopaswa kulindwa na kila Mtanzania.

Akizungumzia Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara hiyo aliyoiwekea Jiwe la Msingi na Miradi mingine ya Maendeleo ni matokeo ya kuwepo kwa Amani na kuiwezesha Serikali kutekeleza Mipango ya Maendeleo.

Ametoa Wito kwa Watanzania Kuendelea kulinda Amani Ili Taifa lipige hatua zaidi za Maendeleo na kwa kuwa huu ni Mwaka wa Uchaguzi amewataka kutumia haki yao kuchagua Viongozi na kuhakikisha Uchaguzi hauwi chanzo cha kuhatarisha Amani ya Nchi na kuweka Mbele Maslahi ya Taifa.

Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Ujenzi , Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Jerry John Silaa alisema Barabara Hiyo itaifungua Wilaya ya Kigamboni Kiuchumi na kuwaunganisha Wananchi katika harakati za Kijamii.

Barabara Hiyo itagharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 83.8 hadi kukamilika kwake inajengwa na Kampuni ya Estim Construction Limited.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here