Rais Mwinyi awaapisha viongozi aliowateua

0

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya aliowateua hivi karibuni.

Hafla hiyo imefanyika leo, Julai 3, 2025, Ikulu ya Zanzibar.

Walioapishwa ni Hamida Mussa Khamis (Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja), Cassian Gallos Nyimbo ( Mkuu wa Wilaya Magharibi ‘A’) na Rajabu Rajab Ali Rajab (Mkuu wa Wilaya ya Kati, Unguja).

Miza Hassan Faki (Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba), Mohamed Ali Abdallah (Mkuu wilaya Mjini, Unguja), Amour Yussuf Mmanga (Mkuu wa Wilaya Magharibi ‘B’, Unguja) na hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vikosi vya Ulinzi na Usalama, pamoja na viongozi wa dini, wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here