Rais Mwinyi amuapisha Makamu wa Pili wa Rais Z’bar

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Hemed Suleiman Abdulla ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa mara ya pili katika Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hafla ya uapisho imefanyika leo, Novemba 8, 2025, Ikulu Zanzibar, na imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wa dini, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka SMZ na SMT, pamoja na wanafamilia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here