Rais Mwinyi akutana na Tony Blair

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemshukuru Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza ambaye pia ni Muwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Tony Blair Institute for Global Change (TBI), Sir Tony Blair kwa ushirikiano wake katika sekta mbalimbali ikiwemo kuimarisha bandari, utalii na kuwajengea uwezo Taasisi ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Serikalini (PDB).

Rais Dkt.Mwinyi alisema hayo alipozungumza na Waziri Mkuu Mstaafu huyo, alipomtembelea kwenye makazi yake The South Pavillion, Cotton Underwood Aylesbury, Uingereza Aprili 6, 2025.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amemuhakikishia kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utafanyika kwa amani na utulivu katika kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu Tony Blair amemuahidi Rais Dkt. Mwinyi kuendelea kushirikiana na Zanzibar katika uchumi wa kidigitali, utalii, uwekezaji kupitia Taasisi yake ya TBI.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na MipangoDkt.Saada Mkuya, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe.Mbelwa Kairuki, Balozi John Ulanga, Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here