RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Septemba 6, 2025, amefungua rasmi Michezo ya Majeshi Tanzania katika Uwanja wa Mao Tse Tung, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema michezo hiyo ni alama ya mshikamano na umoja wa vyombo vya ulinzi nchini, huku ikichangia kuimarisha afya, mshikamano wa kijamii, nidhamu na uchumi.
Ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya michezo kwa kujenga viwanja vya kisasa vinavyokidhi viwango vya CAF na FIFA, sambamba na kuendeleza michezo kama fursa ya uchumi na utalii.
Halikadhalika, amewapongeza wakuu wa vyombo vya ulinzi kwa kuendeleza michezo hiyo tangu ianzishwe mwaka 1977, na kuwataka washiriki kuzingatia mshikamano na umoja.
Michezo ya mwaka huu imeshirikisha kanda saba za JKT, Ngome, SMZ, Uhamiaji, Magereza, Zimamoto na Polisi.