Rais Dkt. Mwinyi amuumbua mwanasiasa mpotoshaji

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, ameelezea kushangazwa na kauli za upotoshaji zinazotolewana mwanasiasa ambaye hakumtaja jina.

Dkt. Mwinyi alisema, yupo mwanasiasa mmoja ambaye anapotosha umma kwa kudai kwamba, Benki ya PBZ inataka kuuzwa, jambo ambalo halina ukweli wowote.

Alisema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Hatifungani za Zanzibar SUKUK, ambazo zipo wazi kwa watu wa imani zote ili kutimiza lengo la Serikali kuwaletea maendeleo watu wake.

Aidha, mpango huo unalenga kufanya iwepo nchini taasisi ya fedha ambayo itaweza kuikopesha Serikali na wawekezaji wenye mahitaji makubwa kifedha katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

Inaelezwa, fedha zitazowekezwa zitakuwa na tija kwa waliowekeza kupata faida ya asilimia 10 mara mbili kwa mwaka na baada miaka 7 mtu anaweza kuchukua amana yake.

“Kuna mwanasiasa anasimama jukwaani na kuwaambia wananchi eti benki ya PBZ ambayo imeanzishwa na Mzee Karume, Serikali inakusudia kuiuza,” alisema Rais Mwinyi.

Aliongeza kuwa, hamuelewi mwanasiasa huyo anasema hivyo kwa kuwa hajui au ni jahili tu, ni mtu mjinga, lakini kwa kuwa kazi ya kiongozi kuelimisha basi ataendelea kufanya hivyo.

Alisema, muda mrefu Serikali imekuwa ikitegemea fedha za mikopo ya nje na za wahisani, jambo ambalo SMZ inapambana kuondokana nalo.

Fedha zitakazo hatifungani hizo ambazo hazina riba zitaijengea uwezo benki hiyo ambayo hivi sasa ipo kukopesha wajasiriamali pekee badala ya Serikali na wafanyabiasha wakubwa na wawekezaji kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesema, ingawa Rais Mwinyi hakumtaja mwanasiasa huyo kwa jina wala chama chake, lakini wanaamini anayekusudiwa Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar Ismail Jussa Ladhu.

Jussa kwa siku za karibunu amekuwa akidaiwa kupanda majukwaani kupotosha na kudanganya umma kuhusiana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here