Posta yashiriki uzinduzi wa wiki ya Simba

0

SHIRIKA la Posta Tanzania likiwa mmoja wa wadhamini wa Wiki ya Simba Day, limeshiriki kikamilifu katika uzinduzi wa Wiki hiyo uliofanyika mkoani Iringa Agosti 30, 2025.

Ushiriki huu ni sehemu ya dhamira ya Shirika katika kuunga mkono matukio makubwa ya kijamii na michezo nchini, huku likitumia fursa hiyo kuongeza muonekano wa huduma zake kwa Watanzania kupitia mshikamano na wadau mbalimbali.

Moja ya shughuli muhimu zilizofanyika katika uzinduzi huo ni tukio la kutembelea Hospitali ya Mafinga, ambapo Simba Sports Club imeonyesha mshikamano wake na jamii kwa kugharamia ujenzi wa jengo jipya lenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 20.

Jengo hili litakuwa msaada mkubwa kwa familia zinazopoteza wapendwa wao, kwa kuwa litahudumia ndugu na jamaa wanaosubiri huduma za hospitali pindi wanapokumbwa na misiba.

Kwa kushiriki katika tukio hili, Shirika la Posta linaendeleza dhima yake ya kuwa kiunganishi cha jamii, si tu kupitia huduma za mawasiliano na usafirishaji, bali pia kwa kushiriki katika shughuli zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Ushirikiano huu unadhihirisha msimamo wa Shirika katika kuchangia maendeleo ya jamii na kuunga mkono jitihada za taasisi na klabu kubwa nchini zinazoweka mbele maslahi ya Watanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here