Posta yajizatiti usambazaji wa jezi za Simba ndani na nje ya nchi

0

SHIRIKA la Posta Tanzania limeungana na mashabiki wa Timu ya Simba kusherehekea uzinduzi wa jezi mpya za klabu hiyo kwa msimu wa 2025/2026, katika hafla maalum iliyofanyika katika ukumbi wa Superdome jijini Dar es Salaam.

Posta ni miongoni mwa wadhamini rasmi wa Simba SC kwa msimu huu na inajivunia kuwa mshirika muhimu katika usambazaji wa jezi hizo kote nchini ambapo kupitia mtandao mpana wa Shirika la Posta litawezesha mashabiki wa Simba walioko maeneo mbalimbali ikiwemo nje ya nchi kupata jezi kwa urahisi, salama na kwa wakati kupitia huduma yake ya EMS.

Jezi mpya za Simba SC zinapatikana katika ofisi zote za Posta Tanzania kwa bei ya Shilingi 32,000 kwa ununuzi wa jumla na Shilingi 45,000 kwa rejareja.

Katika hafla hiyo, Shirika liliwakilishwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Amwesiga Kamihanda kwa niaba ya Postamasta Mkuu, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Ferdinand Kabyemela pamoja na maofisa waandamizi wa Shirika.

Shirika la Posta linaendelea kujizatiti kuwa mtoa huduma wa kisasa na wa uhakika kwa Watanzania na wateja wake duniani kote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here